Na.Salum Msangi,Dar es Salaam.
Maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanywa nchi nzima na Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA yaliyokuwa yanafahamika kwa jina la UKUTA yamesitishwa kwa muda wa Mwezi mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe amesema kuwa wameamua kuahirisha maandamano hayo mara baada ya kuombwa na viongozi wa dini nchini.
"Mimi
ni miongoni mwa watu ambao tulitamani kesho watu wawe barabarani,
wanachama wetu ambao watakwazika, UKUTA sio CHADEMA, UKUTA ni
mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya watanzania. Sasa hayo makundi yamekuja kutushauri tuwe pamoja, sisi ni nani tukatae. Watu kama Mwl Nyerere foundation wametusihi, hata Lowassa amaengea na mama Maria Nyerere wametusihi."Mbowe.
Mh.Mbowe amesema kuwa uamuzi huo wa kusitisha maandamano hayo ya UKUTA
nchi nzima yamewapa wakati mgumu kwakuwa sio kila kitu kinachoamuliwa
kinawapendeza wanachama, lakini anaamini kuwa wanachadema watatuelewa
kwa hili.
"Sio kila wakati viongozi tutafanya mambo yatayowapendeza wanachama wetu, Viongozi wa dini awali walikuja na ajenda moja, kuomba wabunge wa UKAWA warejee bungeni, Kamati kuu ya CHADEMA imepokea kwa heshima sana wito wa viongozi wa dini.
Kufuatia harakati za Operesheni UKUTA
ambazo zimekuwa zikiendendelea kwaajili ya kufanikisha azma yao, Mbowe
amesema kwa Mpaka jana wamekuwa na viongozi 230 amabao wameshtakiwa,
huku viongozi 28 mapaka jana wakiwa hawajaachiwa kwa mujibu wa takwimu
walizonazo wakijumuisha na Naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu.
Hata
hivyo mbowe amesikitishwa na kitendo cha watu ambao anawaita ni
Mahasimu wao ambao wamekuwa wakijaribu kuwagombanisha ndani ya CHADEMA.
" Hizi fitna za mitandao mbowe sina tabia ya kutoa matakamko nje ya taratibu za chama, Tamko nililotoa ni la leo"Amesema Mbowe.
Viongozi
wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa
Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na
serikali.
Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi
walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza
demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa."
"Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama hicho kilisema.
Licha ya katazo la Serikali juu ya Maandamano hayo yalipewa jina UKUTA kwa maana ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania, CHADEMA
haikuogofya na hivyo ikawa ikijiimarisha kwaajili ya Septemba 1, kwa
kufanya vikao kila pembe ya Tanzania vikiwamo vya vya ndani ambavyo
vilipigwa marufuku na Polisi, kitendo kilichopelekea viongozi wengi wa
chama hicho kushikiliwa na Jeshi la Polisi.
Operesheni UKUTA ilikuwa ni muunganiko wa baadhi ya vyama vya upinzani nchini Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment