Katika
ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kushindwa kwa jaribio
la mapinduzi mwezi uliopita, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki
anatarajiwa kukutana na Rais Vladimir Putin mjini St. Petersburg leo.
Hapo jana, Erdogan alisema ziara hiyo ni alama mpya katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Rais huyo wa Uturuki amesema anataka kuanza tena upya uhusiano wa kijeshi, kiuchumi na kiutamaduni.
Uhusiano
wa Uturuki na mataifa ya Ulaya na Marekani umeathirika wakati
serikali mjini Ankara ikifanya msako dhidi ya maelfu ya wanaodaiwa
kuwa waungaji mkono wa jaribio hilo la mapinduzi lililoshindwa.
Uhusiano
na Urusi ulichafuka baada ya Uturuki kuiangusha ndege ya
kijeshi ya Urusi karibu na mpaka na Syria mwezi Novemba mwaka
jana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment