Wataalam
hamsini wa masuala ya usalama ambao kwa pamoja wamewahi kuhudumu katika
utawala wa Republican wameonya kwamba Donald Trump"atakuwa rais asiekua
makini zaidi " kuwahi kuhudumu katika historia ya Marekani.
Katika waraka wao wa wazi wanasema Bwana Trump "hana haiba, maadili wala uzoefu " wa kuongoza nchi.
Kundi
hilo la wataalam wa masuala ya usalama linajumuisha mkurugenzi wa
zamani wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA Michael Hayden na wakuu wa
zamani wa usalama wa ndani wa nchi.
Wengi wa waliotia saini waraka huu kuhusu Trump walikataa kusaini waraka kama huo mwezi Machi.
Bw
Trump amejibu kwa kusema kuwa waraka huo ni wa wasomi wa Washington
waliofeli ambao amesema wanapaswa kulaumiwa kwa kufanya dunia kuwa
mahala hatari.
Bw Trump amekiuka sera ya kigeni ya Republican mara kadhaa.
Mgombea
wa chama cha Republican amehoji ikiwa Marekani inapaswa kuheshimu
wajibu wake kwa NATO, kuidhinisha mateso na kupendekeza kwamba Korea
Kusini na Japan wanapaswa kujihami kwa silaha za nyuklia .
"Alithoofisha
mamlaka ya Marekani inayojitambua kama kiongozi wa dunia huru ,"
ulieleza waraka wa wakuu hao wa zamani wa usalama.
"Anaonekana kukosa
uelewa wa kimsingi kuhusu imani katika katiba ya Marekani, sheria za
Marekani na taasisi za Marekani ,ikiwemo uhuru wa kidini, uhuru wa
vyombo vya habari, na uhuru wa mahakama. ."
"Hakuna hata mmoja wetu atakaempigia kura Donald Trump," ilielezea barua.
Katika
kauli yake Bwana Trump amesema majina ya wale walioandika waraka huo
yalikua "ya wale ambao wamarekani wanapasa kuwatafuta kupata majibu ya
kwanini dunia imeharibika".
"Tunawashukuru kwa kujitokeza ili kila
mmoja nchini atambue ni nani anapaswa kulaumiwa kwa kuifanya dunia kuwa
mahala hatari kiasi hiki ," aliendelea.
" Si lolote hao zaidi ya
wasomi walioshindwa kazi ambao wanataka kuendelea kushikilia mamlaka na
ni wakati sasa wa kuwawajibisha kwa vitendo vyao."
Pia miongoni mwa
wale waliotia saini waraka huo ni pamoja na John Negroponte, mkurugenzi
wa kwanza wa idara ya ujasusi na baadae naibu waziri wa mambo ya nje;
Robert Zoellick, ambae pia alikuwa naibu waziri wa mambo ya kigeni na
rais wa zamani wa Benki ya dunia ; na mawaziri wa zamani wa usalama wa
ndani ya nchi , Tom Ridge na Michael Chertoff.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment