FISI na mbweha wamekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya
Ilemela, ikielezwa kwamba wamekuwa wakiingia katika makazi ya watu na
kushambulia mbuzi, matikitimaji na kabeji kwenye mashamba ya wakulima.
Uchunguzi umeonyesha kuwa wanyama hao ambao wameongezeka maradufu
katika kipindi hiki cha kiangazi, wamekuwa wakizurura na wakisikika
wakitoa milio yao kati ya saa 1.00 usiku na saa 12.30 asubuhi jambo
ambalo limeleta hofu kuhusu usalama wao.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, maeneo ambayo wanyama hao wameonekana
zaidi ni Igoma, Kishili, Kakebe, Mahina, Sahwa, Kanindo, Majengo Mapya
, Fumagila, Bukaga ambako mbuzi wa wananchi wanne wamekwisha kuliwa
pamoja na kuharibiwa mashamba ya matikitimaji na kabeji.
Kuwapo fisi hao kwa wingi kumeleta hofu nyingine kwa ndugu wa
marehemu waliozikwa na wanaoendelea kuzikwa katika makaburi ya Igoma
kwamba yanaweza kufukuliwa na fisi hao ikizingatiwa yamekuwa yakichimbwa
kina kifupi baada ya eneo la maziko kujaa.
Katika makaburi ya eneo hilo, baadhi ya marehemu wamekuwa wakizikwa
juu ya wengine na Halmashauri ya Jiji la Mwanza tayari imetafuta eneo
la Kanindo, Majengo Mapya kama mbadala ya makaburi hayo.
Hata hivyo, bado haijatoa fidia kwa wamiliki wa ardhi hiyo ili yaanze kutumika.
Gazeti hili jana lilitembelea mashamba ya wakulima wa matikitimaji
katika bonde la mto Kishili unaopeleka maji yake Ziwa Victoria na
kushuhudia uharibifu uliofanywa na wanyama hao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakulima wa mashamba
hayo, walisema wanashangazwa na wingi wa fisi na mbweha katika maeneo
yao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment