BARAZA la Taifa la Usalama Barabarani Tanzania limezindua mkakati wa miezi sita kukabiliana na ajali za barabarani.Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema mkakati huo utahusu mambo
14 ikiwamo kudhibiti abiria ambao hawafungi mikanda ya usalama
wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri.
Akizindua mkakati huo Dar es Salaam jana, alisema mkakati huo umeanza kutekelezwa kuanzia jana.
Mkakati huu utakuwa mwiba hususan kwa mabasi yanayofanya safari zake
ndani ya miji maarufu kama ‘daladala’ ambazo nyingi huwa hazina mikanda
ya abiria na hata inapokuwa nayo, abiria hawalipi kipaumbele suala la
kuitumia, alisema.
Alisema katika miezi sita itahakikishwa sheria za usalama
barabarani na ile ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na
Majini (Sumatra) zinafanyiwa marekebisho kuongeza makosa ya barabarani
yakiwamo yanayowagusa abiria moja kwa moja.
“Katika mkakati huu tutadhibiti abiria ambao hawafungi mikanda ya
usalama wanapokuwa katika vyombo vya usafiri, wakati huohuo, tunaendelea
kufanya mchakato wa kurekebisha sheria ya usalama barabarani na ile ya
Sumatra ili abiria ambaye atafanya kosa aweze kushtakiwa,” alisema
Masauni.
Alitaja mambo mengine katika mkakati huo kuwa ni kuanza utaratibu wa
mfumo wa nukta katika leseni za udereva na kudhibiti usafirishaji wa
abiria kwa kutumia magari ya muundo wa tairi moja nyuma mfano Noah.
Nyingine ni kudhibiti madereva walevi na wazembe, kudhibiti mwendo
kasi, uendeshaji wa magari bila sifa, ajali za pikipiki na usafirishaji
wa abiria.
Alisema kwa madereva watakaofanya makosa yanayosababisha madhara
makubwa hawatapigwa faini tu bali watawekwa mahabusu kwa saa 24 kabla ya
kupelekwa mahakamani na kulipa faini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment