Mwendesha mashine kubwa akiwa kwenye mashine yake(Picha na Maktaba).
Serikali
imewataka wananchi kufika ofisi za madini zilizopo kwenye mikoa yao
ili kupewa elimu ya uanzishaji wa shughuli ya uchimbaji wa madini.
Akizungumza ofisini kwake Afisa kaimu wa madini mkoa wa Morogoro ATHUMANI KWALIKO amesema lengo la serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo na watengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotumia madini kupewa ruzuku.
Amesema
ruzuku hiyo itatolewa hata kwa wanaohitaji kuanzisha shughuli za
uchimbaji wa madini na utengenezaji wa vito mbalimbali.
Aidha Afisa KWALIKO amewataka wakazi wa Morogoro kujitokeza kujaza fomu zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuwawezesha vifaa vya kufanyia kazi za madini hatua ambayo itasaidia kutoa ajira na kuliingizia pato taifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment