SPIKA
wa Bunge, Job Ndugai, amesema yuko tayari kuanzisha mazungumzo ya
kurejesha umoja ndani ya Bunge, kutokana na hivi karibuni kutokea
mpasuko katika ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, na wabunge wa upinzani.
Spika
Ndugai, ambaye wakati mtafaruku huo unatokea alikuwa nje ya nchi kwa
ajili ya matibabu, alisema katika kutekeleza hilo, itampasa atafute
baadhi ya watu ambao anaamini wana uzoefu kulifanikisha na kwamba
watakuwa ni watu kutoka katika lililokuwa Bunge Maalum la Katiba na
baadhi ya watu, wakiwamo maspika wastaafu.
Hata hivyo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amelipokea wazo la Spika Ndugai kuongoza upatikanaji suluhu na kusema linakaribishwa, ingawa alitoa angalizo katika utekelezaji wake.
Mbowe alisema Upinzani unaona tatizo katika kutumia maspika wastaafu kwa sababu wote wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo itakuwa ni vigumu kutoa ushauri ambao utakuwa sawa kwa wote.
Kwa mtazamo wa Mbowe, Ndugai anapaswa kuwatumia pia wazee wastaafu kutoka vyama vya upinzani wenye busara na hekima katika kutatua jambo hilo.
Wasiwasi wake ni kuwa mara nyingi viongozi wa CCM linapokuja suala la utaifa wanakuwa upande wa Serikali, akitolea mfano mtafaruku uliotokea bungeni mwaka juzi kuhusu Katiba mpya, lakini walikaa kimya.
Tunampongeza Spika Ndugai kwa kuahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo kwa kuwa unaweza kushusha hadi ya Bunge na vilevile kuwaathiri zaidi wananchi ambao waliwachagua wabunge wa Upinzani ambao wamekuwa wakisusia vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika.
Uamuzi huo bila shaka ameuchukua baada ya kuona Bunge haliendi sawa kutokana na upande mmoja kuona hautendewi haki wakati mhimili huo upo kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa.
Kwa kuwa Ndugai ameliona hilo, tunaamini atawateua watu wa kumsaidia kusaka mwafaka wenye uzoefu, busara, hekima, umakini, uzalendo, weledi na wanaotanguliza mbele maslahi ya taifa badala ya vyama vya siasa.
Ushauri wetu ni kwamba pande zote zikubali kwenda katika meza ya mazungumzo kupata suluhu kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kumaliza tatizo.
Pande zote pia zijiepushe kutoa masharti kwa ajili ya mazungumzo hayo, isipokuwa zitoe maoni na mapendekezo ambayo chanya ambayo yatasaidia kufanikisha mazungumzo hayo.
Wasiwasi alioeleza Mbowe ni sehemu ya mapendekezo kwa Spika kwa ajili ya kumsaidia wakati wa kuwapata watu ambao anaamini kuwa watamsaidia kusimamia mazungumzo hayo.
Kadhalika, pande husika hazinabudi kutambua kuwa hiyo ni fursa pekee ya kufikia maridhiano na kuitumia vizuri kwa kuwa Watanzania wote wanahitaji uwakilishi mzuri katika mhimili wa Bunge.
Wapigakura wengi wameathirika kutokana na wawakilishi wao kutoitumia fursa ya Mkutano wa Tatu wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 kuchangia mipango mbalimbali ya maendeleo ya watu wao pamoja na kueleza kero.
Kukosekana kwa michango yao hakukuathiri wapigakura wao pekee, bali taifa zima kwa kuwa wabunge wa Upinzani wana mchango mkubwa wa kukosoa sera na utendaji wa Serikali na kuibua madudu mbalimbali katika usimamizi na matumizi ya rasilimali za umma.
Ni matarajio yetu kwamba pande zote zitampa ushirikiano Spika Ndugai ikiwa ni pamoja na kuwakubali wapatanishi, kushiriki vikao na kufikia mapatano kwa lengo la kulifanya Bunge kuendelea kuwa chombo kikuu cha kuwasemea na kuwatetea wananchi.

0 comments:
Post a Comment