Baraza
la Sanaa la Taifa (Basata) limemfungulia Msanii wa muziki wa kizazi
kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego kuendelea na
shughuli za Sanaa baada ya kuwa ametekeleza adhabu (maagizo) zote
alizopewa kama masharti ya kumfungulia.
Vilevile
Basata kama mlezi wa wasanii linamfungulia kufuatia yeye mwenyewe (Nay
wa Mitego) kujutia na kukiri kwamba amejifunza na yuko tayari kubadilika
na kwamba hatarudia makosa aliyoyafanya.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngeneza umeeleza
kuwa pamoja na kumfungulia kuendelea na shughuli za Sanaa Baraza
linamweka kwenye uangalizi maalum msanii huyo kama sehemu ya kuhakikisha
anaendesha shughuli za Sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu
sambamba na kuzingatia maadili katika kazi zake.


0 comments:
Post a Comment