BAADA ya Thierry Henry kuchaguliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya
taifa ya Ubelgiji, kocha huyo amedai kuwa nafasi hiyo itamfanya aje kuwa
bora zaidi.
Timu hiyo kwa sasa ipo chini ya kocha wa zamani wa klabu ya Everton,
Roberto Martinez, ambapo kocha huyo ameamua kumpa nafasi nyota wa zamani
wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry.
Awali, Henry alikuwa anaifundisha timu ya vijana ya Arsenal chini ya
miaka 18, lakini aliachana nayo baada ya kupishana kauli na kocha mkuu
wa klabu hiyo, Arsene Wenger.
Henry amedai kuwa alikuwa hawezi kukataa ombi la Martinez kumtaka
kuwa msaidizi wake na anaamini nafasi hiyo itamfanya awe bora katika
ukocha kwa kipindi kifupi kijacho.
“Naanza kwa kukishukuru chama cha soka nchini Ubelgiji na kocha
Martinez kwa kunipa nafasi hii, ninaamini hii ni changamoto kwangu
katika kazi ya ukocha.
“Kitu ambacho tunatakiwa kukifanya ni kuhakikisha ubora wa timu ya
Ubelgiji unabaki pale pale na kuhakikisha inakuwa timu bora zaidi
duniani.
“Nilikuwa namjua vizuri Martinez tangu siku za nyuma, hivyo ilikuwa
ngumu kwangu kukataa ombi lake. Ninaamini nitaweza kufanya kile ambacho
anakitaka na kumsaidia kuipeleka mbali timu hiyo.
“Ninaamini timu hiyo itakuwa na historia mpya kutokana na uwezo wa kocha mkuu na uongozi wake,” alisema Henry.
Mbali na kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, pia ni mchambuzi wa masuala ya michezo katika kampuni ya Sky Sport nchini England.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment