Na.Mwandishi wetu,Dar es Salaam.
..............................................................................................................................
Wakati nchi ikiwa katika giza nene la kipindi cha mwezi mmoja kuanza kwa maandamano ya vyama vya siasa licha ya kukatazwa na vyombo vya dola kwa kile kinachoelezwa kuwa nikuzuia mikusanyiko isiyoyalazima ambayo inaweza kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani nchini huenda likawa na mkwamo.
Chama cha Demokrasia CHADEMA chenyewe kimeazimia kuwa ifikapo Septemba mosi kitafanya maandamano nchi nzima ya Operesheni UKUTA, ambapo 22 Agosti 2016 nao UVCCM
wameibuka nakusema kuwa watafanya maandamano nchi nzima kuunga mkono
juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano jambo ambalo
limeonekana kuwa gumzo kila kona juu ya maandamano hayo.
Wakati vyama
hivyo vya siasa vikijiandaa katika maandamano yenye katazo la dola,
hatimaye kila kona ya nchi Jeshi la Polisi limeonekana likiwa linafanya
mazoezi katika sehemu yenye mikusanyiko ya watu hali ambayo baadhi ya
maeneo watu walikimbia kwa taharuki huku wakishindwa kujua kunani mpaka jeshi linajiimarisha kiasi cha
kukabiliana na na maadui vitani,huku jeshi hilo likisema linajiweka
sawa tu, ambapo wachambuzi wa mambo na hata watu mbalimbali wakisema
kuwa mazoezi hayo huenda yakawa yakukabili Operesheni UKUTA ya chadema inayotarajiwa kuifanya Septemba mosi mwaka 2016.
Wakati wa Mazoezi yapolisi wamekuwa pia wakisisitiza kuwa nivyema wananchi ifikapo Septemba Mosi kila mtu ajitulize kwake kuliko kufanya mikusanyiko isiyoruhusiwa kisheria kwani kufanya hivyo nikwenda kinyume na matamko yanayotolewa na jeshi hilo.
Wananchi
kwa mitazamo tofauti wapo ambao wanaona nivyema vyama vya siasa
vikaachwa vifanye mikusanyiko hiyo kwa kueleza kile walichonacho huku
wengine wakisema kuwa hakuna haja nivyema tu watulie wafanye mambo
mengine yenye maslahi na taifa ili kuepusha umwagaji damu usiowalazima
katika maandamano hayo kwani haifai kushindana na chombo chadola ambacho
kimeoa katazo hilo.
Leo 23 Agosti 2016 Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi amezungumza na wanahabari
kuelezea namna wanavyotazamia mara baada ya matamko ya maanbdamano ya
vyama vya siasa ambayo yanatazamiwa kufanywa na vyama husika licha ya
katazo la kufanya mikutano ambalo limetoplewa na dola.
Jaji Mutungi amesema kuwa kuhusu kufanyika ama kutokufanyika kwa maandamano ya vyama vya siasa
mazungumzo ya vyama vya siasa ya tarehe 29 Agosti2016 na 30 ndiyo
yatakayo amua uwepo wa mikutano hiyo iliyo tangazwa na vyama vya siasa
kwa tarehe tofauti.
Hata hivyo baadhi ya viongozi mbali mbali wa ngazi za juu sambamba na viongozi wa dini wamekuwa wakipaza sauti zao kutaka kuwepo kwa mazungumzo na kuacha kuoneshana ubabe usio na tija ilihali taifa ni moja hivyo yafaa kila mmoja asikilizwe kusudi taifa liweze kufikia lengo linalo taraji haswa kipindi hiki cha serikali ya viwanda.
Taarifa zaidi baada ya muda tutawaletea.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment