Tatizo la uvimbe kwenye mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama
'fibroid.' Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.
Tatizo hili linawakuta wanawake wengi hasa walio katika umri wa miaka
ya uzazi, kimsingi tatizo hili limekuwa likishuhudiwa na watu wengi
pengine kutokana na watu wanavyoishi.
Tatizo hili pia huwa na
dalili zake na miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kuhisi maumivu ya
kiuno hasa wakati wa hedhi, kupata maumivu makali ya tumbo na kuhisi
maumivu waati wa tendo la ndoa.
Dalili nyinyingine ni kutokwa
damu isiyo ya kawaida wakati wa hedhi na zisizokuwa na mpango, kuhisi
maumivu ya mgongo na kupata haja ndogo mara kwa mara kutokana na uvimbe
kukandamiza kibofu cha mkojo.
Mbali na dalili hizo pia dalili nyingine ni pamoja na kutotunga mimba au mimba kuharibika na kutoka, na wakati mwingine ugumba.
Tatizo hili la uvimbe kwenye mfuko wa uzazi 'fibroids' huweza
kusababisha mwanamke kushindwa kupata mtoto kwasababu uvimbe huu
unapokuwa sana hukandamiza mirija ya kupitisha mayai kutoka kwenye ovari
au sehemu mayai yanapotengenezwa. Uvimbe huu pia unaweza kuzuia yai
lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi. Pia hufanya mfuko wa kizazi
ukaze na hivyo kushindwa kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya
kupitisha mayai.
Tunapaswa kujua kuwa wanawake wengi wana
'fibroids' ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina dalili ni ngumu
kufahamu. Kwa mantiki hiyo tunashauriwa kuwa na mazoea ya kufanya
uchunguzi wa afya zetu mara kwa mara ili kuweza kushughulikia haraka
matatizo kama haya.
Moja ya matatizo ambayo huleta huzuni na
uchungu ndani ya familia ni pamoja na hili swala la familia kushindwa
kubahatika kupata watoto.
Hali hiyo hupelekea huzuni ndani ya
nyumba, chuki, lawama, kejeli na kushutumiana na kusababisha hata talaka
pia kati ya wanandoa
Lakini leo nimeona nianze kuzungumzia hili
tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi jambo ambalo mwishowe hupelekea
ugumu wa mama kushika ujauzito.
Matatizo ya kuziba mirija hutokea
pale mwanamke anapopata maambukizi ya mara kwa mara ukeni
yanayoambatana na muwasho kutokwa na uchafu na usaha ukeni, maumivu
wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
Maambukizi hayo huwa na nafasi kubwa ya kusababisha mirija kuziba na ikiwa nje ya mirija husababisha mirija kujikunja.
Maambukizi haya yasipotibiwa kikamilifu huenea hadi katika mfuko wa
uzazi na kushambulia tabaka la ndani la kizazi na kusababisha tatizo
liitwalo ‘Endometriosis’ ambapo mwanamke hulalamika maumivu ya chini ya
tumbo au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na
dalili nyingine zenye kufanana na hizo.
Dalili ambazo huashiria
mwanamke tayari amepatwa na tatizo hili la mirija kuziba ni pamoja na
mwanamke kutafuta ujauzito kipindi kirefu bila mafanikio.
Pia mwanamke mwenye shida hii mara nyingi huwa na kawaidia ya kupatwa na maumivu chini ya tumbo kwa muda mrefu.
Dalili
nyingine ni kuharibika kwa mimba mara kwa mara au kuzaa mtoto mmoja
kisha unapotafuta mwingine huwa inakuwa ni kazi ngumu kumpata tena.
Home
Afya
Slider
Haya ndio matatizo ambayo huchangia baadhi ya wanawake kushindwa kushika mimba kirahisi
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment