Pilipili hoho unaweza kuiweka kwenye kundi la mbogamboga, lakini pia si
vibaya ukiweka hata kwenye kundi la viungo ambacho huweza kuliwa baada
ya kupikwa au hata ikiwa mbichi hususani kwenye kachumbari.
Miongoni mwa virutubisho vinavyopatikana ndani ya hoho ni pamoja na
vitamin C pamoja na collagen ambayo husaidia kulinda afya ya ngozi,
lakini pia vitamin C husaidia kujenga kinga za mwili.
Aidha, ndani ya hoho pia kuna madini mbalimbali ikiwa ni pamoja na
madini ya chuma, calcium, copper, magnesium, zinc pamoja na kiwango
kidogo cha selenium.
Hoho pia ina kiwango cha 'fiber', hivyo husaidia kuboresha umeng'enyaji wa chakula tumboni.
Mbali na hayo, hoho pia husaidia kupunguza kiwango cha cholesterol
mwilini kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'antioxidants' ambacho
husaidia kushusha kiwango cha cholesterol mwilini.
Hoho ni kiungo kizuri kwa wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito wa mwili kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha 'calorie'.
Hupunguza uwezekano wa matatizo ya mfumo wa hewa, hii ni kutokana na
kuwa na utajiri wa vitamin C pamoja na 'antioxidants' ambavyo husaidia
kurekebisha mfumo wa upumuaji.
Huimarisha kinga za mwili, hii ni kutokana na kuwa na kiwango cha
vitamin C ambayo kwa kiasi kikubwa hufanya kazi ya kuboresha kinga za
mwili ndani ya miili yetu.
0 comments:
Post a Comment