Leo tumeamua kuzungumzia jambo hili ambalo huwakumba watu wengi sana katika familia zao, wengi wamekuwa wakitokewa na jambo hili katika mimba zao za kwanza na mimba zao zinazoendelea katika familia zao na kushindwa kupata watoto.
Kuna
wengine wanapata watoto au mtoto mmoja na baadaye wanashindwa kupata
mtoto kwa sababu ya mimba zao kuwa zinaharibika mara kwa mara.
Kwa kawaida kitabibu inaaminika kwamba asilimia 50 ya mimba zote huwa zinaharibika,
najua watu wengi wanaweza wakashangaa lakini ni kweli tafiti za
kitabibu zinasema hivyo isipokuwa watu wengi huwa hawaelewi au wanawake
wengi huwa hawaelewi kama mimba zao zimeharibika kwani hutoka au
huaribika kabla wao hawajagundua kama walikuwa wajawazito.
Isipokuwa wale ambao hujua kwamba walikuwa na ujauzito na umetoka hao wanaweza kuwa asilimia 10 hadi 20, na hizo asilimia zinazobaki kama 35 ni kwa wale ambao hawajui kama mimba zao zimeharibika au walikuwa wajawazito.
Kwa
maana hiyo basi wewe ambaye unatafuta ujauzito kwa muda mrefu sasa na
umekuwa haupati lakini unakuwa unaandamwa na matatizo ya hedhi kwa mara
kadhaa halafu hedhi inakaa sawa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba mimba
zako zimekuwa zikiharibika pasipo wewe kujua.
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
Ni
vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na
uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi
wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa
hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika
hadi wiki ya 20. Na dalili hizo ni kama;
Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba,
pale mwanamke anapopata ujauzito basi ni vema kabisa kujua kwamba
hatakiwi kabisa kupata hedhi au kutokwa na damu katika via vyake vya
uzazi, kwa maana hiyo basi wewe mwanamke ambaye umepata ujauzito na bado
unaona damu inatoka kidogokidogo basi ni vema kuwahi mapema kituo cha
afya kabla tatizo halijawa kubwa kwani kutoka kwa mimba (miscarriage)
huwa hakutokei ghafla tu huanza taratibu na dalili yake kubwa ni hii
kutokwa na damu ilihali wewe ni mjamzito.
Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito,
na wakati mwingine mwanamke anaweza akakumbwa na kutokwa na damu
nyepesi na kabla hajatahamaki, damu ile nzito inaanza kutoka tena, na
hii ni dalili mbaya sana ya kwamba ujauzito wako uko kwenye hatari zaidi
na kuna uwezekano ujauzito ulionao ukatoka, kwa maana hiyo basi
mwanamke anapopatwa na dalili ile ya kwanza ni vema zaidi kufuata
ushauri wa daktari ili kuulinda ujauzito wako.
Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo,
kwa wewe mwanamke ambaye mimba bado ni changa na unapatwa na maumivu
makali sana ya mgongo au kiuno au vyote kwa pamoja basi ni vema kuwahi
kituo cha afya ili kuangalia ni jinsi gani unaweza kuzuia ujauzito wako
usitoke au usikumbwe na tatizo hili la kutokwa na ujauzito
(miscarriage).
Kama
unapatwa na dalili kama hizi kutokwa na damu nyepesi au nzito ilihali
wewe ni mjamzito basi ni vema kuwahi kituo cha afya au wasiliana nasi
ili kukusaidia. Kwa ushauri vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye
vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.
Sorry can I have your contact so as we can communicate
ReplyDelete