Ezekiel
Kemboi, amepokonywa medali ya shaba aliyoishindia nchi yake ya Kenya
katika mbio za Mita 3000 kuruka viunzi na maji katika michezo ya
Olimpiki nchini Brazil siku ya Jumatano.
Hatua hiyo ilichukuliwa na
Shirikisho la riadha duniani IAAF, baada ya kubainika kuwa alikimbilia
nje ya eneo maalum kwa mujibu wa kanuni za riadha baada ya Ufaransa
kulalamika.
Baada ya uamuzi huo Mfaransa Mahiedine Mekhissi aliyemaliza nafasi ya nne, alitunukiwa medali hiyo ya shaba.
Kemboi
mwenye umri wa miaka 34 na bingwa mara mbili katika Michezo ya Olimpiki
mwaka 2004 na 2012 amehuzunishwa na hatua hiyo baada ya kutangaza kuwa
anastaafu riadha.
Hata hivyo, Kenya iliendeleza rekodi yake ya
kunyakua medali ya dhahabu katika mbio hizi baada ya Conseslus Kipruto
kuibuka bingwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment