Hamza,
mtoto wa Osama bin Laden, mwanzilishi wa al-Qaeda ametoa wito wa
kuuangusha utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia. Wito huu ameuelekeza
hasa kwa vijana ambao wamechoshwa na utawala wa Kifalme nchini Saudi
Arabia kujiunga na kundi la Al-Qaeda, mjini Yemen.
Wakati wa uhai
wake, Osama Bin Laden alitaka kumfanya mtoto wake, Hamza, ambaye kwa leo
ana umri wa miaka 23, mrithi wake katika uongozi wakundi la Al-Qaeda.
Kwa
mujibu wa nyaraka zilizothibitishwa, inaonekana kuwa Hamza bin Laden
anasikilizwa na kuheshimiwa katika safu ya wanajihadi kuliko Ayman
al-Zawahiri, mrithi wa baba yake tangu Mei 2011.
Tishio kwa Saudi Arabia na marekani
Mtoto
aliyekua akipendwa sana na Osama bin Laden amewataka vijana wa Saudi
Arabia, na wale wenye uwezo wa kupambana, kujiunga na kundi la AQPA
lenye mafungamano na Al-Qaeda, lililoanzishwa mwaka 2009 kwa kuungana
kati ya makundi mawili kutoka Saudi Arabia na nchini Yemen.
Miaka
mitano baada ya kifo cha mratibu mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11,
2001 nchini Marekani, jina la Bin Laden limeanza kusikika tena kama
tishio la kweli kwa Saudi Arabia na Marekani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment