Aliyekuwa Makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar ameondoka katika ardhi ya Sudan Kusini kufuatia machafuko yaliyoanza tangu mwanzoni mwa mwezi Julai katika mji mkuu Juba. Machar kwa sasa amekimbilia katika "nchi salama" ya ukanda wa Afrika mashariki, mmoja wa maafisa waandamizi kutoka kambi yake.
Riek Machar sasa amehamishiwa katika nchi salama ya ukkanda wa Afrika mashariki, amesema Mabior Garang de Mabior, msemaji wa SPLM-IO, chama cha Bw Machar, katika taarifa yake usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi.
Bila kutoa maelezo zaidi kuhusu eneo alikokimbilia Bw machar, msemaji wa chama cha SPLM-IO pia amehakikisha kwamba muhusika, ambaye yuko mafichoni tangu kuanza kwa mapigano mwezi Julai, atazungumza katika mkutano na waandishi wa habari ndani ya masaa 24 yajayo, ameongeza Bw Garang de Mabior.
Machar alikimbilia mafichoni kutoka mji wa Juba wakati wa mapigano makali katika mji huo Julai 8 na 11 kati ya vikosi vya Rais Salva Kiir na ewanajeshi wanaomuunga mkono Riek Machar. Nafasi ya Riek Machar kwa sasa inasikiliwa na mshirika wake wa zamani Taban Deng Gay.
Kiir na Machar wamekua wakitupiana lawama kuhusu mapigano ya mwezi Julai, ambayo wamehatarisha mkataba wa amani uliyoafikiwa mwezi Agosti mwaka 2015. mkataba wenye lengo la kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilioanza mwezi Desemba 2013 na ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na watu milioni 2.5 kuyahama makazi yao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment