Aliyekuwa
Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika
Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.
Kiongozi
huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini
Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini
Jumapili.
"Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani
hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati
mwafaka," taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema.
Desemba mwaka
2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani
wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.
Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment