Msanii wa bongo fleva,Dullayo ambaye amewahi kutamba na vibao vyake
kama naumia roho na mida ya kazi amelalamikiwa na majirani kwa kukithiri
kwenye tabia ya ulevi jambo ambalo linamfanya ashindwe kufanya vizuri kisanaa kama alivyokuwa mwanzo na ikizingatiwa hivi sasa music ni ushandani na alishakuwa na jina zuri kupitia muziki.
Wakiongea kwenye kipengele cha Cheche kinachopatikana kwenye kipindi
cha E-Newz cha East Africa TV kinachozungumzia maisha ya mastaa wakiwa
mtaani,majirani hao ambao wengi walimsifu Dullayo kwa kutokuwa na
maringo kama mastaa wengine walisema tatizo la msanii huyo ni Ulevi hivyo akiacha ama kupunguza ulevi kitamsaidia na atafanya vizuri katika muziki kama wanavyofanya wengine.
“Kusema kweli Dullayo ni
msanii mzuri,mdogo wetu,tunaishi naye vizuri katika mtaa wetu lakini
kitu kimoja Dullayo anatuudhi anakunywa sana pombe na msanii anapokunywa
saana pombe badaye anakuja anaharibika” Kutokana na
msanii huyo kuwa na jina baadhi ya washkaji wamemshauri kufanya namna ya
kuinua vijana wenzake ambao nao wanafanya muziki ili mwisho wa siku
wainuke kama wanavyofanya wasanii wengine kuwainua wanamuziki chipukizi
katika mitaa yao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment