KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog, amewahakikishia mashabiki
wa timu hiyo kuwa kikosi hicho kitanyakua ubingwa wa michuano ya Ligi
Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Omog alitoa kauli hiyo kutokana na timu hiyo kuanza vyema Ligi Kuu
kwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa ufunguzi
uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Omog alisema mikakati yao katika
kufanikisha lengo la kutwaa ubingwa ni kuhakikisha wanashinda kila
mchezo watakaocheza kwenye ligi hiyo.
Alisema Simba imesajili wachezaji wengi wenye uwezo hivyo atawapa
mbinu za kupambana uwanjani na kuwajengea morali wakati wa mazoezi na
mechi zinazowakabili.
“Tunaendelea kuboresha safu ya ushambuliaji na ukabaji ili tufanye
vizuri zaidi katika mchezo ujao dhidi ya JKT Ruvu,” alisema Omog.
Kocha huyo aliyewahi kuinoa Azam FC kabla ya kutua Simba, aliongeza
kuwa wanaendelea na juhudi za kukisuka kikosi hicho ili kiweze
kukabiliana na timu yoyote ya Ligi Kuu.
“Tuna muda wa kutosha kujipanga, kesho tunaendelea na mazoezi huku
tukijitahidi kwa nguvu zote kuiweka timu katika hali nzuri ya kupambana
kwenye mechi inayofuata,” alisema Omog.
Akizungumzia hali ya afya ya beki wa timu hiyo, Hamad Juma, aliyepata
ajali hivi karibuni, Omog alisema anaendelea kupata matibabu akiwa
mapumzikoni mkoani Tanga.
Home
MICHEZO
Slider
Omog, amewahakikishia mashabiki wa Simba ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment