Image
Image

Erdogan akutana na naibu rais wa Marekani Joe Biden katika ikulu jijini Ankara

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimkaribisha naibu rais wa Marekani Joe Biden katika ikulu na kufanya mkutano wa mazungumzo.Joe Biden aliwasili jana jijini Ankara kutekeleza ziara rasmi kwa ajili ya kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na Uturuki.
Katika mazungumzo yao, rais Erdogan aliitaka serikali ya Marekani kuchukuwa hatua ya kumrudisha Uturuki Fethullah Gulen ambaye ni kongozi wa kundi la FETO.
Erdogan alielezea mautamini yake aliyokuwa nayo kuhusu suala hilo na kutarajia Marekani ichukuwe hatua haraka iwezekanavyo.
Akizungumzia suala la DAESH, Erdogan alisema, ‘‘Mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la DAESH ni suala muhimu. Hatuwezi kutenganisha makundi ya kigaidi. Hatuwezi kuruhusu yaendelee kutishia usalama wa taifa.’’
Joe Biden naye alitoa maelezo na kusema, ‘‘Hatuna sababu yoyote ya kumlinda kiongozi wa kundi la FETO Fethullah Gulen.’’
Biden pia alikumbushia kwamba Marekani imekuwa ikiunga mkono serikali ya Uturuki tangu siku ya kwanza ya jaribio la mapinduzi na kusema,
‘‘Marekani iko tayari kusaidia katika suala la hukumu dhidi ya wahaini wote wa jaribio la mapinduzi. Vile vile uamuzi kuhusiana na suala la kumrudisha Gulen Uturuki pia utatolewa hivi karibuni. ’’
Akielezea kwamba Marekani haitorudi nyuma katika suala la mapambano dhidi ya ugaidi, Biden alisema, ‘‘Wananchi wa Marekani wapo pamoja na Uturuki na rais Barack Obama ni mmoja wa viongozi waliofanya mawasiliano. Laiti ningezuru Uturuki hapo awali.’’
Biden akiwa na kamati ya wajumbe kutoka Marekani kwa mara ya kwanza wamefanya ziara katika bunge la Uturuki huku wakiwa na nia ya kuboresha mahusiano na Uturuki baada ya jaribio la mapinduzi.
Katika ziara yake ya bungeni, Biden alikutana na mwenyekiti wa bunge  İsmail Kahraman.
Kahraman alimshukuru Biden kwa ziara yake bungeni ya kutoa pole kwa Uturuki.
Joe Biden aliweza kuona hasara iliyotokea baada ya FETO kulipua eneo moja la Bunge usiku wa jaribio la mapinduzi la Julai 15 .
Baada ya hapo naibu rais huyo alielkea katika ikulu ya Çankaya ambapo alikutana na waziri mkuu Binali Yildirim na kufanya mazungumzo.
Waziri mkuu Binali Yildirim ametoa maelezo na kuarifu kwamba harakati za kijeshi zinapaswa kuendeshwa katika maeneo ya mpakani mwa Syria kutokana na tishio la makundi ya kigaidi ya DAESH na YPG.
Waziri mkuu Yildirim alitoa maelezo hayo kwenye mahojiano aliyofanya na baadhi ya vituo vya televisheni.
Akisisitiza kwamba makundi ya kigaidi yanayohusiana na PKK hayatopewa fursa ya kutekeleza harakati zao katika eneo la Wakurdi, Yildirim alisema kuwa kundi la PYD halina njia nyingine isipokuwa kutorokea upande wa mto Firat ulioko mashariki.
Yildirim pia alikumbushia umuhimu wa kulinda ardhi ya Syria na kuonya kwamba hali inaweza kuzorota zaidi endapo kila jamii ya kiasili itathubutu kuunda taifa lake katika kanda hiyo.
Katika maelezo yake, Yildirim pia aliarifu serikali ya Uturuki kuwa tayari kushirikiana na Marekani, Urusi na Iran katika suala la kujenga Syria mpya itakayounganisha jamii zote na kuishi kwa amani na utulivu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment