Image
Image

Mwanamke wa Kipalestina asimamishwa kazi kwa kujitanda hijab nchini Ujerumani

Mwanagenzi mmoja mwenye asili ya Kipalestina ameripotiwa kufukuzwa kazini siku ya kwanza kwa kujitanda hijab katika jimbo la Brandenburg nchini Ujerumani.Mwanagenzi huyo mwenye umri wa miaka 48 aliyeanza kazi alipigwa kalamu na meya wa mji wa Luckenwalde Elisabeth Herzog von der Heide.
Meya Heide alitoa maelezo na kuarifu kuchukuwa hatua dhidi ya hijab kwa sababu taasisi za serikali kama ofisi za manispaa zinapaswa kuwa za kawaida na wazi kwa umma.
Heide aliendelea kukashifu vazi la hijabu kwa kudai kuwa linaashiria upande maalum wa jamii maalum duniani na kusisitiza kutokuwepo kwa hata ishara za misalaba ndani ya ofisi za manispaa.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Heide alilazimika kumuondoa mwanagenzi huyo wa Kipalestina aliyeanza kazi katika ofisi ya manispaa inayohusu wakimbizi iliyotarajiwa kuchukuwa wiki 6 kutokana na kukataa kuvua hijab alipokuwa katika mazingira ya wanaume.
Kwa upande mwingine, mwanachama wa bunge la Brandenburg wa chama cha Kikristo cha CDU Sven Petke alikosoa uamuzi wa Heide na kusema kwamba ni kinyume cha sheria.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment