Mwimbaji wa bongo fleva Kassim Mganga amefunguka na kusema kuwa
maisha mengi ya wasanii wa muziki huo hayako kama vile wanavyoonyesha
kwenye mitandao.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa,Kassim amedai watu
wasanii wengi huiga wasanii wa nje kuonyesha maisha ya kifahari bila
kujua kuwa wenzao ndio maisha yao ya uhalisia hivyo ni kama wanadanganya
mashabiki.
“Kitu ambacho nimejifunza,
wenzetu hawa’act, wenzetu wako real, ndio maisha yako vile, ukimuona
Chris Brown au ukimuona 50 Cent pamoja na umri wake aliokuwa nao leo,
anaonesha magari yake,ni kwa sababu watu wapo kwenye ushindani wa
biashara kubwa sana, kwa hiyo anachokifanya kina mantiki, sisi tumekuwa
tuna’fake vitu vingi havipo real, lakini tunataka tuwaoneshe kwenye
mitandao, tunadanganya, tunawadanganya sana mashabiki wetu, mashabiki
wanatuona si watu ambao tuna maisha makubwa sana, wakati haiko hivyo
kiuhalisia“, alisema Kassim Mganga.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment