Na.Salum Msangi,Dar es Salaam.
..............................................................................................
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba amesema
kuwa yeye ni Mwenyekiti halali wa CUF kwani tayari amekwisha muandikia
barua msajili wa vyama vya Siasa nchini Bw.Francis Mutungi kwa ajili ya
kumjulisha kwamba alitengua barua yake ya kujiuzulu uenyekiti wa CUF mwaka jana na pia alisha mueleza Katibu Mkuu wa chama hicho cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad kwamba alitaka kuanza kazi rasmi kuanzia June 10 mwaka huu lakini katibu huyo alimueleza kuwa anatafuta ushauri wa kisheria ambapo mpaka hivi leo hajapewa ushauri huo wa Kisheria.
Kauli
hiyo ya Profesa Lipumba anaizungumza zikiwa ni sa kadhaa tangu wavuliwe
uanachama wa CUF na Baraza Kuu la Chama hicho lililofanya mkutano wake
visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwajadili wanachama kadhaa wakiwemo
vigogo hao.
"Sisi hatukupewa taarifa yeyote, hatujapewa taarifa
ya tuhuma na wala taarifa ya hukumu iliyotolewa tumesikia kwenye vyombo
vya habari,taarifa hiyo sisi hatuikubali"Amesema Lipumba.
Katika
kuzungumzia kilicho amuliwa na Baraza kuu la CUF Ibrahimu Lipumba
amesema kuwa uamuzi huo hauna mashiko kwani kikao hicho hakikuwa na
uhalali hata chembe, kwakuwa Naibu Katibu mkuu Bi.Magdalena Sakaya
ambaye ndio msaidizi mkuu wa Katibu Mkuu hakuhusishwa kabisa katika
kikao hicho kilicho toa maamuzi na hawakuwapo wajumbe wakutosha kutoka
Tanzania bara hivyo kikao hicho sio kikao rasmi wala sihalali.
Kuhusu
Prof.Lipumba kutokuelewana na Maalim Seif amesema kuwa, Katibu mkuu
huyo amekuwa akikiendesha chama hicho cha CUF ndivyo sivyo kwani amekuwa
hampi heshima inayostahili Naibu Katibu Mkuu, hamshirikishi katika
mambo mbalimbali kutoka bara ambaye kikatika ndiye msaidizi wake mkuu
kwani utaratibu huo umekuwa sio mzuri.
"Maalim Seif anambagua
Naibu Katibu Mkuu,anafanya maamuzi bila hata kumshirikisha huu sio
utaratibu mzuri, huu ni utaratibu wa kiimla"Amesema Lipumba.
Prof.Lipumba
ameenda mbali zaidi huku akisema kuwa kwa hivi sasa vyama vyote vya
kidemo Krasia havikai hata kidogo nakuanza kupanga kuwafukuza uanachama
wanachama wao.
"Ukiwa unafukuza wanachama unajitangaza wewe kwamba nichama cha KIDIKTETA, chama cha KIIMLA kwahiyo sisi tunahitaji chama cha kuwa sawa kwa wote, chama ambacho kinafuata misingi mizuri ya Demokrasia"Amesema Lipumba.
Mara
baada ya Baraza kuu la CUF kumteua Bw.Julius Mtatiro kuwa Mwenyekiti wa
chama hicho kwa muda wakati taratibu zingine zikiendelea, Lipumba
amesema kuwa ndani ya chama hicho Mtatiro hawezi kupewa nafasi hiyo
nyeti.
"Julius Mtatiro
sio Mwenyekiti wa Muda, Julius Mtatiro nilimteua mimi kuwa mjumbe wa
mkutano Mkuu, hana uanachama wowote yule,na mimi ndio nimemuingiza hata
kwenye kamati ya utendaji, kwahiyo Mtatiro hawezi kuwa Mwenyekiti
ameshindwa hata kukiondoza kikao cha Mkutano Mkuu na ndio maana vurugu
ikatokea"Amesema Lipumba.
Aidha
Prof.Lipumba amesema kuwa licha ya kadhia hizo zinazojitokeza ndani ya
chama lakini Chama hicho anawahakikishia wanachama wake kuwa kipo imara,
waendelee kukienzi na kuwataka wawe na subira kwani Mwenyekiti wao yupo
imara na sasa yupo ngangari kinoma, kwani suala linaloelezwa kuwa
ametenguliwa uanachama hazina ukweli kwakuwa kikao hicho kilikuwa
sihalali cha kumtengua, kwani yeye ameteuliwa na Mkutano Mkuu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment