Siku moja baada ya kufungiwa kwa muda kwa vyombo viwili vya habari, Radio Five ya mkoani Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaam, wadau wa habari wamekuwa na maoni tofauti kuhusu uamuzi uliotangazwa na Serikali.
Akitangaza
uamuzi huo Jumatatu ya wiki hii jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari,
Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amesema amefikia uamuzi
huo baada ya kujirdhisha kuwa kipindi vipindi vilivyorushwa na vituo
hivyo kati ya Agosti 25 na Agosti 17 mwaka huu vilikuwa na maudhui ya
uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Waziri Nape amesema kuwa
amevifungia kwa muda usiojulikana vituo hivyo kwa kukiuka masharti na
kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na
c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.
Wakati
vyombo hivyo vya habari vikifungiwa, baadhi ya wadau wa habari
walioongea na idhaa hii wamekuwa na mtazamo tofauti, huku baadhi
wakiunga mkono kwa kile wanachosema kuwa katika miaka ya hivi karibuni,
vipindi vingi vya redio vimekuwa havina maudhui chanya yenye kuleta
chachu ya mabadiliko kwa jamii, na badala yake vimekuwa vikihamasisha
mgawanyiko na kutengeneza chuki.
Wadau hao wameenda mbali zaidi na
kudai kuwa umefika wakati, taaluma ya uanahabari ichukuliwe kwa umakini
mkubwa hasa na wamiliki wa vyombo hivyo kwa kuhakikisha kuwa watangazaji
wao wanazingatia maudhui mazuri ya vipindi vyao ili kuepusha kupotosha
uma ama kutengeneza mazingira ya uchochezi.
Wapo pia wadau ambao
wanapinga uamuzi huu wa Serikali kwa kile wanachosema kuwa vyombo vya
habari viko huru katika kutoa mitazamo ya kile ambacho kimejiri katika
jamii, ama kiwe na muonekano hasi au chanya isipokuwa wazungumzaji wake
wamezingatia weledi kwa kuzungumza kile ambacho kimezungumza na
kujadiliwa.
Wadau hao wametolea mfano vipindi vya hivi karibuni
vilivyowahi kurushwa kwenye runinga na redio kukosa maadili huku kamati
ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano ikivifumbia macho vipindi hivyo
ambavyo vilichukiza watu wengi na hata kuzua mjadala mkali kwenye
mitandao ya kijamii.
Waziri Nape, akatumia furas ahiyo kuvionya
vyombo vingine vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na kanuni
zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda taaluma hiyo.
Home
News
Slider
Serikali kuvifungia vituo vya habari viwili Tanzania,wadau wamekuwa na mtizamo tofauti.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment