TUMECHOKA kuvumilia! Ni kauli ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kudai kusakamwa na Serikali .
Chama
hicho kimetoa kauli hiyo leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, baada ya Jaji Mstaafu, Salome Kaganda ambaye ni Kamishna wa
Maadili na Mtendaji Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
kuwaandikia barua viongozi wa chama hicho akiwatuhumu “kukiuka masharti
ya Hati ya Ahadi ya Uadilifu wa Viongozi wa Umma.”
Jaji Kaganda
aliwaandikia barua viongozi hao tarehe 4 mwezi huu ambapo Chadema
wameitaka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuacha vitisho kwa
viongozi wa chama hicho.
Walioandikiwa barua hiyo ni Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema na Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.
Vincent
Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, kwa mujibu wa barua ya Jaji
Kaganda, katika tarehe, muda na siku ambayo haijulikani, viongozi hao wa
Chadema walitoa matamshi ambayo yanachochea wananchi kutotii sheria,
kufanya vurugu, kudharau misingi ya demokrasia iliyopo nchini na
kutishia usalama wa nchi.
“Hata hivyo, Jaji Kaganda hakuyataja
matamshi hayo wala kuyafafanua. Aidha, alidai kwamba matamshi hayo
yanatokana na maazimio yaliyofikiwa na kikundi cha watu wachache nje ya
Bunge,” amesema Dk. Mashinji.
Licha ya kudai kwamba, maazimio ya
kikundi hicho yanapuuza utangamano, utulivu na usalama wa wananchi
wengine kinyume na dhana ya maslahi mapana ya umma, Jaji Kaganda
hakukitaja kikundi hicho cha watu wachache nje ya bunge huku pia akidai
matamshi ya viongozi hao yalilenga ‘kushamirisha ‘ maslahi yao binafsi
na maslahi ya Chadema.
“Mheshimiwa Mbowe ni Mwenyekiti wa Taifa wa
chama kikuu cha upinzani hapa nchini. Ni kiongozi wa chama ambacho
mgombea urais wake alipata zaidi ya kura milioni sita kati ya kura 15
milioni zilizopigwa kwenye uchaguzi mkuu wa urais mwaka jana.
“Ni
mbunge wa kuchaguliwa na kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Katika
Bunge. Ni mtu na kiongozi anayejulikana na kuheshimika ndani na nje ya
Tanzania. Kusema kuwa kiongozi huyo anaongoza kikundi cha watu wachache
nje ya Bunge kwenyewe ni kuonesha maadili yenye mashaka kwa mwandishi wa
barua hiyo,” amesema Dk. Mashinji.
Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki ameeleza kushangazwa na barua ya Jaji Kaganda akisema;
“Ni
vigumu kuamini kwamba, barua hii imeandikwa na mwanasheria na mtu
ambaye amewahi kushikilia madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
“Barua ambayo haina maelezo yoyote ya kile kinachodaiwa kuwa kosa; haitaji tarehe, siku, muda au mahali kosa hilo lilipotendeka.
“Haitaji
vifungu vya sheria yoyote iliyokiukwa na wala kuonyesha kama
sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma ina mamlaka kisheria ya
kushughulikia kosa hilo, in onyesha mapungufu makubwa ya kitaaluma na
kiuandishi ya kamishna wa maadili na katika mazingira ya kawaida,
ingestahili kupuuzwa,” amesema Lissu.
Kwa mujibu wa Lissu ambaye ni
mwanasheria wa chama hicho, Chadema haiwezi kuipuuza barua hiyo na
kwamba, inaashiria kuwepo kwa njama za kuwafungulia mashtaka katika
Mahakama ya Maadili Viongozi hao ambao ni wabunge kwa lengo la kuwavua
ubunge.
Aidha, mojawapo ya vigezo vya kikatiba vya mtu kukosa sifa ya
kuwa mbunge ni pamoja na kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa
kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya
maadili ya viongozi wa umma.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, kamishna wa
maadili ana mamlaka ya kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya
viongozi wa umma na kuunda mahakama (Tribunal) ya kusikiliza tuhuma hizo
na kupeleka taarifa ya mashauri hayo kwa kamishna ambaye atapaswa
kuwasilisha nakala za taarifa hiyo kwa rais na spika wa Bunge.
“Rais Magufuli na washauri wake wanafahamu ugumu wa kutumia mahakama za kawaida kwa lengo la kukandamiza wapinzani.
“Licha
ya matatizo yake mengi, Mahakama ya Tanzania imedhihirisha mara nyingi
uwezo wa kulinda uhuru wake na kutokuwa tayari kutumika kwa malengo ya
kisiasa ya watawala.
“Sasa Magufuli (Rais John Magufuli) na washauri
wake wanaandaa mazingira ya kuitisha Mahakama ya Kangaroo
watakayoidhibiti wao ili kuhakikisha wanawakandamiza viongozi wakuu wa
chama chetu.
“Kama ambavyo tumethibitisha mara kwa mara chama chetu
hakitakuwa tayari kuona viongozi wake wakikandamizwa kwa kutumia kivuli
cha maadili ya viongozi wa umma. Tutapambana na njama hizo. Kwa uthabiti
na kwa weledi ule ule ambao tumepambana na njama nyingine za aina hiyo
katika siku za nyuma,” ameeleza Lissu.
Aidha Jaji Kaganda amenukuliwa
na gazeti la Mwananchi la leo akikana kujua kuhusu barua hiyo huku
akisema “mimi sifahamu kuhusu suala hilo, sina taarifa.”
Home
News
Slider
Lissu: Barua ya Sekretarieti ya Maadili ni njama ya kutengeneza mazingira ya kisheria kunivua Ubunge.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment