Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemtangaza
Bw.Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji
Mkuu wa Serikali kuanzia Agosti 5 Mwaka huu.
Uteuzi huo umefanyika
kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 kifungu
Namba 6(1)(b) kufuatia uhamisho wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo
Bw. Assah Mwambene uliofanyika tarehe 7 Machi 2016 kwenda Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe.Nape Moses
Nnauye ametoa wito kwa Wanahabari na Wananchi kwa ujumla kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Bw Abbas atakapokuwa anatekeleza majukumu
yake.
“Ninawaomba Wanahabari na Watanzania kwa ujumla mumtambue Bw
Abbas na mtoe ushirikiano unaostahili katika utendaji wa kazi
zake”.Alisema Mhe. Waziri.
Aidha Mhe. Waziri Nape alimpongeza Bibi
Zamaradi Kawawa aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo kwa kujituma na
kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu na uadilifu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi huyo mpya amekubali uteuzi huo na ameahidi
kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu mkubwa na ameomba ushirikiano wa
kutosha kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo na Watanzania
kwa ujumla.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Hassan Abbas alikuwa ni Meneja
Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais inayosimamia Utekelezaji wa
Program ya Matokeo Makubwa sasa (President`s Delivery Bureau).
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment