Image
Image

Majambazi wauwa Polisi 4 waliokuwa wakibadilishana lindo Temeke Dar es Salaam.

Askari Polisi wanne wameuawa na wengine kujeruhiwa, baada ya watu wanaoaminika kuwa ni majambazi kuvamia Benki ya CRDB tawi la Mbande Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam jana jioni wakati askari hao wakibadilishana lindo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SIMON SIRO amesema watu kadhaa wamekamatwa na msako unaendelea kuwatafuta wauaji hao walitekeleza mauaji hayo ya sakari.
Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.
Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.
Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.
“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” amesema Kamanda Sirro huku akiwataka watu kujihadhari na yeyote anayejitambulisha kwao kuwa ni askari bila kuonesha kitambulisho.
Ameendelea kusema kuwa baada ya operesheni ya kukomesha mtandao wa wahalifu kama hao na wengine kukimbilia nchi jirani, masalia wameanza kujikusanya na kutekeleza matukio ya mauaji huku askari wakilengwa.

Sauti wa Kamanda wa Polisi Simon Sirro iko hapa akielezea tukio la mauaji ya polisi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment