Jenerali
mstaafu kwenye jeshi la Uholanzi ataongoza jopo huru la uchunguzi
kubaini ikiwa walinda amani wa umoja wa Mataifa walishindwa kuwalinda
raia wakati wa mapigano makali yaliyozuka kusini mwa mji mkuu wa Sudan
Kusini, mwezi uliopita.
Meja jenerali Patrick Cammaert atawasilisha
ripoti ya uchunguzi huo ndani ya mwezi mmoja kwa katibu mkuu wa umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon, ambapo matokeo yake yatawekwa wazi kwa uma,
amesema msemaji wa umoja wa Mataifa.
Vikosi vya umoja wa Mataifa
nchini Sudan Kusini vimejikuta kwenye shinikizo kubwa vikikosolewa kwa
madai kuwa vilishindwa kuwalinda raia wakiwemo wanawake na wasichana
ambao walibakwa jirani kabisa na kambi ya vikosi hivyo kwenye mapigano
ya mwezi Julai mjini Juba.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa umerekodi
visa zaidi ya 200 vya ubakaji vilivyotekelezwa mwezi Julai peke yake na
wanajeshi wa Serikali ambao ni watiifu kwa Serikali ya Rais Salva Kiir.
Mwezi
uliopita, katibu mkuu Ban Ki Moon alitangaza kuwa ataanzisha uchunguzi
huru kuhusu taarifa za walinda amani hao kushindwa kufika kwa wakati
kuwasaidia raia waliohitaji msaada wakati wa mapigano na pia kuchunguza
mashambulizi tofauti kwenye hoteli moja mjini Juba.
Wanajeshi wa
Sudan Kusini wanatuhumiwa kuwabaka wanawake, kuwadhalilisha wafanyakazi
wa umoja wa Mataifa na kumoiga risasi mwandishi wa habari kwenye
shambulio la Julai 11 kwenye hoteli ya Terrain mjini Juba, ambapo
walinda amani hao wanadaiwa kushindwa kufika kutoa msaada.
Uchunguzi
huo utabaini ikiwa walinda amani wa umoja wa Mataifa walioko nchini
Sudan Kusini wanaofahamika kama UNMISS, walidhibiti hali kimaadili na
kuwalinda raia kwa muda muafaka, alisema msemaji wa umoja wa Mataifa,
Stephane Dujarric.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment