JUMLA ya kikosi cha watu 35 ambao ni wachezaji na viongozi wa MO
Bajaia kutoka Algeria, wametua Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Agosti 9,
2016 na imefikia Hoteli ya Ledger Plaza, iliyoko Kunduchi Beach nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Timu
hiyo imekuja kucheza na Young Africans ya Dar es Salaam, katika mchezo
wa nne wa hatua ya Nane Bora kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika
utakaofanyika Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Licha ya kwamba
Young Africans kuwa na pointi moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za
juu katika kundi la A ambalo msimamo wake unaongozwa na TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na
Medeama ya Ghana, zina pointi tano kila moja. Wakati Young Africans
wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria,
Medeama itakipiga na TP Mazembe.
Mchezo
wa Young Africans dhidi ya Mo Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka
Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na
Kindie Mussie mstari upande wa kusini na Temesgin Samuel Atango katika
mstari wa Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus
Bezezew Belete.
Kamishna
wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka
wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa
mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan. Mratibu huyo anatarajiwa
kuwasili leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi watatua kesho Agosti 11,
2016 na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12, 2016.
Kiingilio
katika mchezo huo kitakuwa ni Sh 3,000 kwa mzungunguko kwa maana ya
viti vya kijani, bluu na chungwa wakati Viti Maalumu vyenye hadhi ya
daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A kiingilio kitakuwa
ni Sh 15,000 kwa mujibu wa Waratibu wa Young Africans.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment