Waziri
wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba amewaambia askari wa jeshi la
Polisi mkoani Katavi kufanya kazi kwa taratibu na sheria bila kumuonea
mtu yeyote hasa wanyonge.
Waziri Mwigulu ametoa agizo
hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea makazi ya watanzania wapya
pamoja na kuzungumza na askari wa jeshi la polisi, Magereza pamoja na
Uhamiaji.
Mhe. Mwigulu amesema kuwa Askari hao waondokane na tabia ya matukio ya kuwabambikizia kesi raia kwa maslahi binafsi na kuwaonea na kusema kuwa serikali kali ya awamu ya tano haitamfumbia macho askari atakayebainika kufanya hivyo.
Aidha Waziri Mwigulu amechukua fursa hiyo kuwapa hamasa Askari hao kwa kusema kuwa serikali itawaboreshea maslahi yao kadri bajeti itakavyoruhusu ili waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi.
Home
News
Slider
Waziri nchemba awataka Polisi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria bila kuonea wanyonge.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment