Image
Image

Mwambusi kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika tumejifunza mengi.

KOCHA msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema pamoja na kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini wamepata fundisho kubwa. Yanga iliaga rasmi michuano hiyo juzi baada ya kukubali kipigo cha mbaoa 3-1 kutoka kwa TP Mazembe ya Congo DR katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe mjini Lubumbashi.
Kipigo hicho kinaifanya Yanga iliyokuwa kundi A kwenye michuano hiyo kushinda mechi moja tu kati ya sita ilizocheza.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwambusi alisema hapo walipofika wanamshukuru Mungu kwani michuano ilikuwa migumu na wamejifunza mengi.
“Tunamshukuru Mungu hapa tulipofika kwa sababu kazi haikuwa rahisi, tumejifunza tunarudi kujipanga upya,”alisema.
Alisema wamejifunza mambo mengi na kubwa ni suala la nidhamu ya mchezo na mchezaji uwanjani.
Mwambusi alisema timu yake iliandamwa na kadi akitolea mfano wa baadhi ya wachezaji Donald Ngoma ambaye alikuwa tegemeo kwenye kikosi hicho lakini alionyeshwa kadi za njano na kukosa michezo miwili hali iliyoathiri timu.
Kocha huyo wa zamani wa Mbeya City aliwashukuru mashabiki wa Yanga kwa kuwaunga mkono kipindi chote cha mashindano na kuwahimiza kuendelea kuwa pamoja kutengeneza Yanga mpya yenye ushindani.
Wachezaji wengine wa Yanga waliopata kadi wakati timu hiyo ikishiriki michuano ya kimataifa ni Kelvin Yondani, Vincent Bousou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Amis Tambwe na Mwinyi Haji.
“Watanzania watuelewe kuwa tulipofikia sio haba, tunachoangalia ni namna ya kujipanga upya kwa michezo iliyoko mbele yetu,” alisema.
Yanga sasa inarudi kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo msimu mpya wa mwaka 2016/2017 umeanza tangu wiki iliyopita.
Hata hivyo, pamoja na kutolewa timu hiyo bado itawakilisha tena nchi kwenye michuano ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani ndio mabingwa wa msimu wa mwaka 2015/2016.
Yanga ilitarajiwa kuwasili jana na leo itaendelea na mazoezi ya kujifua kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya African Lyon mwishoni mwa wiki hii.
Yanga imetolewa Kombe la Shirikisho ikiwa inashika mkia kwa pointi zake nne baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya Mo Bejaia, kupata sare ya 1-1 dhidi ya Medeama na kupoteza michezo yote ya ugenini dhidi ya timu hizo na mmoja wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment