Jeshi
la Polisi nchini Tanzania limetolea ufafanuzi juu ya Mazoezi ambayo
jeshi hilo limekuwa likifanya katika Sehemu mbali mbali nchini ambapo
kumekuwa na mitazamo tofauti juu ya mazoezi hayo.
Mazoezi ya Jeshi la
polisi ambayo polisi walisema kuwa wanafanya ili kuimarisha miili
yao,yamekuwa yakihusishwa wa wadau mbalimbali kuwa huenda kwamba mazoezi
hayo niyakujikita kukabiliana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambao wametangaza wazi kuwa Septemba mosi mwaka huu watafanya maandamano nchi nzima yaliyo pachikwa jina la Opesresheni UKUTA.
Katazo
la kufanya mikutano ya maandamano lilitolewa siku za usoni na Rais
Dkt.John Pombe Magufuli na kuwataka wanaotaka kufanya mikutano nibora
wakafanya mikutano hiyo katika majimbo yao kuliko kukusanyana na
kuandamana hali ambayo huenda ikaleta uvunjifu waamani huku akisema
siasa zilishakwisha kilichobaki sasa nikazi tu nas siasa tena ni mwaka
2020.
Kuhusu Katazo hilo limepelekea baadhi ya vyama vya siasa kikiwamo CHADEMA ambapo kimeandaa Operesheni UKUTA,kwa
kuzunguka nchi nzima huku wachambuzi mbalimbali wa mambo wakisema
mvutano huo baina ya serikali kuu na vyama vya siasa yafaa kutazamwa
upya kwani taifa nimoja hakuna haya ya kugombea fito.
Leo 22Agosti 206 kupitia tarifa ya Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera John Bulimba imefafanua juu ya mazoezi ambayo yamekuwa yakifanywa na jeshi hilo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
“Kufuatia
hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu
wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la
polisi.”Amesema Bulimba.
Aidha, jeshi la polisi linawataka
wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo
hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment