Image
Image

Rais MAGUFULI apokea shilingi mil 116 za msaada wa madawati.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuchangia madawati kwa kutoa hundi yenye thamni ya kiasi cha dola za Kimarekani (USD 53,000) kwa ajili ya utengeezwaji wa madawati.............................................................................................................................
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya DAWOODI BOHRA duniani Mtukufu Dakta SYEDNA MUFADDAL SAIFUDDIN SAHEB amemkabidhi Rais JOHN MAGUFULI hundi.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya DAWOODI BOHRA duniani Mtukufu Dakta  SYEDNA MUFADDAL SAIFUDDIN SAHEB amemkabidhi Rais JOHN MAGUFULI hundi ya Dola Elfu 53 za Kimarekani ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 116 za Kitanzania kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shule mbalimbali hapa nchini.
Dakta  SAIFUDDIN SAHEB amekabidhi hundi hiyo Ikulu Jijini DSM alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais MAGUFULI ambapo pia amekabidhi hundi nyingine ya Dola Elfu 23 za Kimarekani ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 46 kwa ajili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania - BAKWATA.
Mazungumzo haya yamehudhuriwa pia na Mufti wa TANZANIA Sheikh ABOUBAKAR ZUBEIR  na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dakta AUGUSTINE MAHIGA ambapo Rais MAGUFULI amewakaribisha wana Jumuiya hiyo kuwekeza hapa nchini.
Rais MAGUFULI pia amewakaribisha Wanajumuiya hao katika Maadhimisho ya Jumuiya ya DAWOODI BOHRA duniani yanayotarajiwa kufanyika Jijini DSM Mwezi Oktoba mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Rais MAGUFULI amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya SAHARAWI, -BRAHIM GHALI iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais BACHIR MOUSTAPHA SAYED.
Pamoja na kupokea barua hiyo Rais MAGUFULI amesema Serikali yake itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiarabu ya SAHARAWI na pia itaendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri hiyo kupata haki ya kuamua hatma yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment