MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa kulifuta shtaka la kutakatisha fedha Sh
milioni 400 linalomkabili mtuhumiwa wa wizi wa Sh milioni saba kwa
dakika, Mohammedi Mustafa na mwenzake.
Uamuzi wa kukataa kulifuta
shtaka hilo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri baada ya
kusikiliza hoja za pande mbili zinazopingana katika kesi hiyo.
Mustafa
na Sammuel Lema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern
Engineering Work Limited wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 222.
Watuhumiwa
hao wanaokabiliwa na kesi ya jinai namba 36 ya 2016, wanadaiwa kutenda
makosa kati ya Februari mosi mwaka 2013 na Desemba 31,2015.
Katika
hati ya mashtaka, kwa pamoja wanadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali za
Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) kuanzia kosa namba mbili hadi 103,
kosa namba 104 hadi 142 yakidaiwa kufanywa na mtuhumiwa wa kwanza,
Mustafa.
Shtaka la 220 ambalo ni la kukwepa kulipa kodi lilifanywa
katika kipindi hicho ambapo mshtakiwa wa kwanza anatuhumiwa kukwepa kodi
ya Sh bilioni 14.
Shtaka la 221 linalohusu utakatishaji fedha
linadaiwa kutendwa na washtakiwa wote wawili, inadaiwa Sh milioni 400
zilitakatishwa kupitia akaunti ya Iqbal Jafareri katika Benki ya IMM
tawi la Kariakoo.
Shtaka la mwisho ni kuisababishia TRA hasara ya Sh bilioni 13 kupitia ukwepaji kodi.
Wakili
Alex Mgongolwa na wenzake wa upande wa utetezi waliwasilisha hoja
kupinga shtaka la 221 la utakatishaji fedha kwa madai kuwa lina upungufu
kisheria ambao hauwezi kurekebishika na kwamba maelezo ya shtaka hilo
hayajitoshelezi.
Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa alipinga hoja hizo kwa madai kwamba mahakama haina mamlaka ya kutoa uamuzi huo.
Akitoa
uamuzi, Hakimu Mashauri alisema mahakama ilisikiliza hoja za pande zote
mbili na katika kufikia uamuzi ilijikita kuangalia mamlaka ya mahakama
kuangalia uhalali wa hati ya mashtaka.
Alisema katika kutetea hoja
zilizowasilishwa kesi mbalimbali za mahakama ya juu na moja wapo
ilishakatiwa rufaa hivyo haiwezi kutumika katika kufikia uamuzi.
“Kesi
iliyopo mahakamani inatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu, inapitia katika
mahakama ya chini kwa ajili yua kusubiria upelelezi kukamilika ihamie
mahakama hiyo ya juu.
“Kwa kuzingatia mipaka hiyo Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kulifuta shtaka hilo la kutakatisha
fedha,”alisema hakimu na kuyatupa maombi ya upande wa utetezi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment