Dodoma. Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NGO’s), Marcel Katemba amesema Serikali haitasita kuyafuta mashirika yanayojihusisha na masuala ya kutetea mapenzi ya jinsia moja.
Katemba alitoa kauli hiyo mjini hapa jana baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa kitaifa wa NGO’s nchini.
“Kwa
mfano hapa nchini hatujasajili shirika hata moja linaloruhusu mapenzi
ya jinsia moja, nasema hivyo kwa sababu yanajua kuwa kitu cha namna hiyo
hakikubaliki, sasa utakuta mashirika haya yanajiingiza kwenye sakata
hilo kutokana na masharti ya kupata fedha yanayotolewa na wafadhili
kutoka nje ya nchi, wanaotaka kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja.
“Serikali
hatujaruhusu mambo hayo nchini, ndiyo maana tukalifuta usajili Shirika
la Sisi kwa Sisi na hatutasita kumchukulia hatua atakayejihusisha na
mambo yaliyo nje ya katiba yake,” alisema.
Alisisitiza
kuwa Serikali italifutia usajili shirika lolote lisilo la kiserikali
litakalofanya kazi zake kinyume na katiba ya nchi.
0 comments:
Post a Comment