Dar es Salaam. Baadhi
ya wananchi wanaotumia king’amuzi cha Star Times wamelalakimikia
kutoonekana kwa chaneli tano za televisheni za ndani ya nchi kwa zaidi
ya miezi miwili, licha ya kutakiwa kuzionyesha bure.
Wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema
awali, walikuwa wakizipata chaneli za ITV, EATV, Star TV, Channel 10 na
TBC1 bila malipo, lakini sasa wanapata TV1 na TBC1 pekee.
Mkazi wa
Mwenge jijini hapa, Razack Kazembe alisema awali alikuwa anapata chaneli
hizo, lakini kwa sasa hazipati na alipouliza kituo cha huduma kwa
wateja cha Star Time aliambiwa anatakiwa kulipia.
Kanuni ya 7(a) ya
Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2011
inazitaka kampuni zenye leseni ya miundombinu ya dijitalali (multiplex
operator) kurusha chaneli tano za ndani bure na inayokiuka inatakiwa
kulipa faini isiyopungua Sh5 milioni.
Meneja Huduma kwa Wateja wa
Star Media, Gasper Ngowi alisema hawajaanzisha utaratibu wa kutoza
malipo chaneli hizo za bure na kuwataka wananchi wasioziona kufika
ofisini kwao.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini
(TCRA), Innocent Mungy alisema wanatambua kuwa StarTimes inatoa huduma
bure kwa chaneli tano za Kitanzania na kwamba uchunguzi ukibaini
taratibu zimekiukwa sheria itafuata mkondo wake.
Source Mwananchi:->http://www.mwananchi.co.tz
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment