Leo asubuhi (Ijumaa, Agosti 26, 2016) Waziri
Mkuu amekutana na viongozi wakuu mbalimbali wa makampuni ya kibiashara
kutoka Japan ambao wamekuja kuhudhuria mkutano huo.
Waziri Mkuu amekutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Chiyoda Corporation, Bw. Tadashi Izawa ambapo katika mazungumzo yao, pamoja
na kuangalia fursa nyingine katika sekta ya gesi Tanzania, kampuni hiyo
imekubali kutoa mafunzo ya kujenga uwezo wa wataalamu kwa sekta ya gesi
hususan usindikaji wa gesi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
(Liquefied Natural Gas).
Bw.
Izawa amemweleza Waziri Mkuu kwamba wamefurahiswa na taarifa za
ugunduzi wa gesi ya Helium hapa nchini Tanzania na kwamba kampuni yake
ina teknolojia na uzoefu wa muda mrefu katika kutekeleza miradi ya gesi (Gas value Chain Planning and Execution).
“Tunao
uzoefu wa muda mrefu, pia tunazo teknolojia za kuendeleza sekta ya gesi
ikiwemo Helium kwa mfano ujuzi wa kutenganisha gesi asilia na helium
(Separation of Natural Gas and Helium). Tumetekeleza miradi ya namna hii
nchini Qatar ambayo kwa sasa ni ya pili kwa uzalishaji wa gesi hiyo
duniani ikitanguliwa na Marekani,” amesema.
Amesema
mafunzo hayo yatafanyika kuanzia mwakani na yatalenga vijana
wasiopungua 10 kutoka Tanzania ambao wamehitimu shahada za uhandisi
kwani wameshafanya hivyo kwa vijana wanane kutoka Msumbiji.
Waziri
Mkuu alimshukuru Vw. Izawa kwa mpango wao wa mafunzo kwa vijana wa
Kitanzania lakini akamtaka pia waangalie uwezekano wa kuwasaidia vijana
wanaotoka maeneo husika yenye gesi ili wapatiwe mafunzo ambayo
yatawawezesha kumudu baadhi ya kazi kwenye viwanda vya kusindika gesi.
Wakati huohuo, Waziri
Mkuu amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la
Misaada ya Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato na kujadiliana
mambo kadhaa yakiwemo ya nishati na miundombinu.
Katika
mazungumzo hayo, Bw. Kato alimweleza Waziri Mkuu nia ya shirika hilo
kuendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kilimo hapa nchini na hasa
katika sekta za afya, maji, kilimo na miundombinu ambazo imekuwa
ikijihusisha nazo kwa muda mrefu sasa.
Waziri
Mkuu alimshukuru kwa ushiriki wa shirika hilo kwenye miradi ya nishati
ya Kinyerezi na akamtaka aendelee kuisaidia Serikali ya Tanzania
inainginia kwenye awamu ya tatu ya Kinyerezi (Kinyerezi III).
Katika
hatua nyingine, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe
alimwoba makamu wa Rais hyo waangalie uwezekano wa kuwekeza kwenye sekta
za nishati na miundombinu ya mkoa Dodoma hasa katika kipindi ambacho
Serkali imeamua kuhamia huko.
“Tunaomba
muangalie sana suala la kuendeleza nishati ya umeme kwani nchi yetu
imeamua kuwa nchi ya viwanda. Tutahitaji kuwa na umeme wa kutosha
kuendesha viwanda vya usindikaji bidhaa zetu, lakini pia si mbaya
mkiangalia suala la kuboresha miundombinu ya barabara na usafirishaji
katika mji wa Dodoma,” amesema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, AGOSTI 26, 2016.
0 comments:
Post a Comment