Serikali
ya Tanzania imewasilisha ombi la kukata rufaa, uamuzi wa kihistoria
nchini uliopinga ndoa za watoto walio chini ya umri wa miaka 18.Mwezi
uliopita mahakama kuu iliamua kuwa sehemu za sheria ya ndoa mwaka 1971,
iliyoruhusu wasichana kuolewa wakiwa na umri wa hata miaka 14 ni kinyume
na katiba.
Kundi la kutetea haki za watoto "Msichana Initiative"
iliwasilisha kesi hiyo mahakamani. Taarifa hiyo ya kukata rufaa
imewashtusha wengi Tanzania , wengi wakishindwa kuelewa ni kwanini mkuu
wa sheria angetaka kugeuza hukumu hiyo.
Mwezi uliopita mahakama kuu
iliipa serikali muda wa mwaka mmoja kurekebisha kosa hilo na kuweka umri
wa miaka 18 kama umri sahihi wa watu kufunga ndoa, kwa wote wasichana
na wavulana nchini.
Awali sheria ya ndoa ya mwaka 1971 nchini
Tanzania imetaja kuwa wavulana wanapaswa kuoa wakiwana miaka 18 huku
wasichana wakiwa na umri wa miaka 15. Kesi hiyo iliwasilishwa na kundi
la kutetea haki za watoto Msichana Initiative, kupitia wakili Jebra
Kambole.
Asilimia 37 ya wasichana walio na umri wa chini huolewa
Tanzania. Wasichana wenye umri wa hata miaka 14 huozwa kwa idhini ya
wazazi. Na wengi wao baadaye huripotiwa kukabiliwa na unyanyasaji
nyumbani na hutengwa katika jamii - wakikosa nafasi za kusoma na
kuajiriwa.
Hivi karibuni bunge lilikarabati kipengee cha sheria ya
elimu na sasa ina sehemu inayotoa hukumu ya kifungo cha miaka 30
gerezani au faini ya dola 2500 kwa wanaume wanaowapachika mimba au
kuwaoa wasichana wa shule.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment