Na Abushehe Nondo na Sheila Simba-Maelezo
Serikali
imesema kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier
Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa
anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya viwanja vya
ndege vilivyopo nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati
wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani katika chuo cha Taifa
cha usafirishaji(NIT)
Mbarawa alisema kuwa Serikali haikukurupuka
katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za kununua badala yake
imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa ndani na
kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
“Serikali
imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali
halisi ya Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa
baadhi, huku lengo ni kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa
Mbarawa.
Mbarawa aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni
kuhudumia wananchi hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani
zimezingatia mambo mbalimbali ikiwemo suala la usalama na ufanisi
katika uendeshaji wake.
Aliongeza kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua
katika viwanja vingi hapa nchini kwani zinaweza kutua katika viwanja
vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ndio vingi nchini tofauti na aina
nyingine ambazo hutua kwenye viwanja vyenye urefu zaidi ya kilomita
mbili.
Prof. Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza
uwezo mdogo wa ndege hizo katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina
zingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa
zikitumia Tani 1.7 za mafuta tofauti na aina nyingine zinazotumia hadi
Tani 2.8 kwa safari moja.
Waziri Mbarawa pia alitumia fursa hiyo
kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni
ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha kuwa suala hilo siyo la kweli
kwani kampuni hiyo imefanya biashara na nchini nyingi ikiwemo Ethiopia
yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400 zilizotengezwa na Kampuni hiyo.
Mpaka
sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa
asilimia 40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19
septemba mwaka huu ambapo zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe
15 septemba mwaka huu kupitia nchini Uingereza.
Akizindua mafunzo
hayo ya wakufunzi wa marubani, Waziri Mbarawa aliwaasa Marubani ambao
watahitimu mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia suala na nidhamu na
uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.
“Hatutaki kuwa na
marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio waadilifu,hakikisheni
mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika
sekta hiyo ya anga ambapo wakati mwingine Rubani anajijua anakasoro
lakini bado anang’ang’ania kurusha ndege” alisema Prof.Mbarawa.
Aidha
amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za
urubani ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini.
Home
News
Slider
Serikali yasema imezingatia vigezo na haijakurupuka kununua ndege ya Bombadier Q400.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment