Wananchi
wa Gabon wanasubiri kutangaziwa matokeo ya uchaguzi wa urais, na wengi
wana hofu ya kutokea kwa machafuko baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo
leo Jumanne. Mshindi hajafahamika, licha ya kila upande kudai kushinda
uchuguzi huo wa Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita.
Rais anaye
maliza muda wake, Ali Bongo Ondimba, anawania kinyanganyiro hiki kwa
muhula wa pili wa mika saba, huku akishindana na Mwenyekiti wa zamani wa
Tume ya Umoja wa Afrika, Jean Ping.
Waziri wa Mambo ya Ndani
anatazamiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi kuanzia saa 11 jioni saa za
Gabon katika majengo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Cenap) wakati ambapo
raia wa nchi hii wanaishi kwa hofu ya kutokea kwa machafuko tangu
kufungwa kwa vituo vya kupigia kura Jumamosi jioni.
Kiongozi wa
zamani wa chama cha majaji wakati wa utawala wa Omar Bongo Ondimba, na
kiongozi wa upinzani baada ya uchaguzi wa mwanawe Ali Bongo mwaka 2009,
Jean Ping, 73, anapania kuipindua familia ya Omar Bongo, madarakani
tangu mwaka 1967 katika ukanda huo wa Afrika ya kati, ambapo kupishana
katika madaraka si rahisi.
"Nimechaguliwa," alisema Jumapili Jean
Ping, wakati ambapo rais anaye maliza muhula wake Ali Bongo anasubiri
kutangzwa matokeo ya uchaguzi, akiwa na imani ya kushinda uchaguzi huo.
Msemaji wake, hata hivyo alitangaza Jumamosi jioni kwamba Ali Bongo
anaongoza kwa kura nyingi dhidi ya mpinzani wake, na hawezi kushindwa.
Utawala
kwa upande wake umesema kuwa unaendelea kuimarisha usalama, huku kambi
ya Jean Ping ikisema hautakubali kuibwa. Hofu ya kutokea kwa machafuko
inaonekana baada kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, kwani kila upande
unadai kushinda uchaguzi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment