Shirika
la kimataifa la Save the Children limetahadharisha kuhusu mlipuko wa
ugonjwa wa homa ya manjano katika nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo na Angola kuwa hivi karibuni unaweza kuenea katika nchi za mabara
ya ulaya , Amerika na Asia.
Ugonjwa huo unaenezwa na mbu aina ya aedes, wanaopatikana katika nchi nyingi za Afrika Magharibi.
Mlipuko
wa ugonjwa huo barani unaelezwa kuwa mkubwa kuliko miaka 30 iliyopita
na umesababisha kutumika kwa chanjo mara nne kuliko ilivyo kawaida kwa
mwaka huu pekee jambo lililofanya Shrika la Afya duniani WHO kupunguza
kiwango cha dozi ili kuwezesha watu wengi zaidi kupata chanjo hiyo.
Shirika
hilo la Save the children limesema limetuma wataalamu wake kusaidiana
na serikali ya DRC kutoa chanjo homa hiyo ya manjano kwa watu nusu
milioni katika mji mkuu wa Kinshasa.
Tayari mzungumko wa kwanza wa
chanjo hiyo ilishatolewa katika mji huo wa Kinshasa baada ya
kuthibitishwa kulipuka kwa ugonjwa huo ambao hauna tiba.
Awali ugonjwa huo uliripotiwa katika nchi jirani ya Angola kabla ya kuenea nchi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Zaidi
ya watu mia nne walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki katika nchi hizo
mbili ambapo huku wengine zaidi ya watu elfu sita wakiripotiwa
kuambukiza ugonjwa huo.
Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema
hakuna maambukizi mapya yaliyoripotiwa nchini Angola tangu mwezi juni ,
na kufufua matumaini kwamba ugonjwa huo sasa utadhibitiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment