Image
Image

Viongozi wa dini waombea amani Tanzania kwa kuweka utaifa mbele Morogoro.

 Na.DevothaSongorwa,Morogoro 
............................................................................................................................................................
Viongozi wa dini zote kwa kushirikiana na viongozi wa serikali wamefanya Kongamamno la kuombea Amani Taifa la Tanzania ambalo limefanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Akizungumza na wananchi Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi Dk KEBWE STEPHEN KEBWE amesema kuwa amani ni ya muhimu katika nchi ili kuwepo kwa usalama wa wananchi na mali zao hivyo ni jukumu la kila mwamnachi bila ubaguzi kujali na kudumisha amani iliyopo.
Amewataka viongozi na watendaji wote wa serikali kuunda kamati ya Amani katika maeneo yao jambo litakalosaidia kutoa elimu na kuhamasisisha jamii kuachana na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ya nchi.
Aidha Dk. KEBWE  amewaonya wale wanaotarajia kufanya maandamano mnamo september mosi mwaka huu kufuatia operesheni UKUTA inayoendeshwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kuacha kufanya hivyo na badala yake wafanye shughuli za kujieletea maendeleo.
Hata hivyo amewaomba wananchi kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa  za mtu yeyote  ambae wana mashaka nae na kuonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani  na amewashukuru
Viongozi wa dini na madhehebu yote mkoani Morogoro  kwa kushirikiana na serikali kuiombea amani nchi.
 Ameitaka Kamati ya Amani mkoani Morogoro kushirikiana na viongozi wa dini zote  kuendelea kutoa elimu kwa jamii kutambua kuwa amani ni msingi wa maendeleo ya taifa na dunia kwa ujumla.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment