Hata
hivyo, kama wadau wa michezo tungependa kuchukua fursa hii kuishauri
TFF kusimamia vizuri ratiba hiyo ili kupunguza malalamiko kama
ilivyokuwa msimu uliopita.
Wote ni mashahidi jinsi msimu uliopita ligi hiyo ilivyoendeshwa kwa malalamiko mengi kiasi cha wadau wa michezo kubaki na maswali mengi ya kujiuliza kuliko majibu.
Usimamizi mbovu, kupanguliwa hovyo ratiba za mechi na malalamiko mengi dhidi ya waamuzi, yaliifanya TFF kuwa kiini cha lawama msimu mzima.
Upanguaji mbovu wa ratiba ndiko kulikoifanya Yanga kumaliza mechi zake nne za mwisho ugenini.
Mbali na kupangua ratiba, pia TFF ilingia katika lawama ya kutoa ruhusa kwa Azam FC kwenda Zambia kushiriki mashindano yaliyofananishwa na 'bonanza' na kuifanya ligi kuwa na mechi nyingi za 'viporo' bila ya sababu za msingi.
Ni jambo la ajabu kwenye ligi timu moja inabaki na viporo vya mechi nne na zote zinachezwa ugenini.
Uamuzi huo wa TFF ulilalamikiwa na wadau wengi wa michezo hasa klabu ya Simba iliyotishia kutopeleka timu uwanjani hadi wapinzani wao Yanga watakapomaliza mechi zao za viporo.
Leo hii tunaamini itajirudia na kusimama kwenye mstari mzuri wa usimamizi wa ligi hiyo ili kurejesha imani kwa mashabiki wa soka.
Tungependa kuona TFF ikijipanga upya na kuendesha ligi katika utaratibu utakaopunguza kama siyo kufuta kabisa malalamiko.
Msimu huu uwe alama ya TFF kujirekebisha kwa yale yaliyotokea msimu uliopita kwa kuendesha ligi vizuri na kuepuka kupangua ratiba bila sababu za msingi.
Tunatambua kuwa ratiba ya safari hii imezingatia kalenda za mashindano ya kimataifa, hivyo hatutashuhudia tena migongano kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Lakini pia tunaamini kuwa, kama TFF itaamua kuondokana na utumwa wa kubeba lawama kila msimu, basi msimu huu itasimamia vizuri kanuni na sheria zake.
Tungependa kuona msimu huu bingwa anapatikana bila kuwapo na manung'uniko wala lawama dhidi ya waamuzi.
Tunafahamu kuwa kwenye ushindani wowote, malalamikao hayawezi kukosekana, lakini haitakuwa na maana kama malalamiko yatakuwa yale yale kila msimu.
Vile vile TFF na kamati zake zinatakiwa kukutana na kutoa uamuzi ripoti za mechi na rufaa mbalimbali ambazo zinawasilishwa na timu kwa wakati ili kujiepusha na tuhuma za 'kuzibeba' baadhi ya timu.
Msimu uliopita tumeshuhudia malalamiko yaliyowasilishwa na Simba kuhusiana na aliyekuwa mchezaji wake Hassan Kessy kupigwa na Donald Ngoma yakiachwa kutolewa uamuzi wowote. Hapo TFF inakosea.
Nipashe, tunachukuwa nafasi hii pia kuzitaka timu zitakazoshiriki michuano hiyo mafanikio mema kuelekea siku ya kwanza ya msimu huu.

0 comments:
Post a Comment