Aliyekuwa
Waziri wa Kilimo na Chakula na Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Stephen Wassira ameomba wasaidizi wa Rais John Magufuli kumshauri
kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kuepusha madhara
yanayoweza kutokea kutokana na maandamano yanayopangwa kufanyika
Septemba 1.
Wassira ameeleza kuwa washauri hao wanapaswa kufanya
hivyo kwani bado nafasi hiyo ipo kuliko kuacha Rais aingie vitani na
wananchi wake kwani madhara yatawapata Watanzania wote.
“Wazungumze
ili wasimuingize Rais kupigana na watu wake kwa maana wote tutapoteza.
Kwa nini uweke askari polisi wote hao, msimweke Rais kwenye vita na watu
wake,” Wassira anakaririwa na Jambo Leo.
“Kinachohitajika ni
wasaidizi wa Rais kumshauri ili kuhakikisha kuwa tofuati zilizopo baina
yake na vyama vya upinzani haziendelei ili kuepusha madhara yanayoweza
kuzuilika, itafutwe suluhu,” aliongeza.
Akizungumzia uamuzi wa
Serikali kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano na maandamano, alisema
kuwa tatizo linaweza kuwa ni aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya
Chadema, Edward Lowassa.
Alisema kuwa hii inatokana na joto la
uchaguzi lililokuwepo pamoja na nia ya Lowassa kuzunguka nchi nzima
kuwashukuru wapiga kura, kungeweza kuzua tafrani kubwa kwani alipata
kura nyingi na alikuwa akidai ameshinda kwa asilimia 62.
“Ukiwaruhusu
kufanya mikutano na ukwaambia kuwa atakayekuja kutoa shukurani ni
Lowassa, ambaye amekuwa akipinga kushindwa ni sawa na kurejesha hali ya
uchaguzi kipindi hiki,” alisema.
Alitaka Serikali kutoa elimu ya wazi kwa umma kuhusu sababu zinazopelekea kukataza kufanyika kwa mikutano ili kuweka mambo sawa.
“Kama
mimi hapa nimetaja sababu kwamba inawezakana kuwa ni Lowassa. Sasa na
wao Serikali waseme tu tunapiga marufuku mikutano na maandamano… wataje
[sababu]na kuzifafanua,” alieleza.
Hata hivyo, Wassira aliwataka
Chadema kusitisha adhma yao na kuhakikisha wanafuata utaratibu ili
kupata haki ya kufanya maandamano na mikutano ambayo alieleza kuwa kila
Katiba ya nchi duniani imeiweka, lakini bila kufuata utaratibu haiwezi
kuruhusiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment