MKURUGENZI
Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Rashid Othman amestaafu rasmi
wadhifa huo, huku akitajwa kuwa miongoni mwa viongozi waliofanya kazi
nzuri wakiongoza taasisi hiyo nyeti.
Habari za uhakika kutoka ndani
ya serikali, zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zilisema kuwa
Othman alistaafu rasmi wadhifa huo Agosti 19, mwaka huu akiwa ameiongoza
taasisi hiyo tangu Agosti 20, 2006 ikiwa ni takribani miaka 10.
Kiongozi
huyo aliteuliwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa
Mkurugenzi Mkuu ili kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkurugenzi
Mkuu wa wakati huo, Cornel Apson Mwang’onda.
Aliapishwa Ikulu Dar es
Salaam Agosti 21, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Othman alikuwa Mkuu wa
Utawala na Utumishi wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa na kufanya kazi
nzuri, iliyochangia kumwezesha kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.
Awali,
Othman alitakiwa kustaafu mwaka 2013 kwa mujibu wa sheria, lakini
aliendelea kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja hadi alipokubaliwa
kustaafu rasmi Ijumaa iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment