Image
Image

Abubakar Shekau,atoa kanda ya video akikana madai ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo kuwa aliuawa.

Kiongozi  wa kundi la Nigeria Boko Haram Abubakar Shekau, ametoa kanda ya video akikana madai ya jeshi  la Serikali ya nchi hiyo kuwa aliuawa au amepata majeraha  wakati wa mashambulizi ya angani mwezi uliopita.
Kiongozi huyo wa kikundi  hicho  cha wapiganaji wa Bokoharamu  ameonekana mwenye afya njema kwenye kanda hiyo ambayo alizungumza kwa lugha za kiarabu, Hausa na Kanuri ili kuweza kufikisha ujumbe kuhusiana na afya yake.
Haijabainika video hiyo ilirekodiwa lini na  jeshi la nchi hiyo ya  Nigeria halijazungumza chochote kile kuhusiana na video hiyo ya Abubakar Shekau.
Mapema mwezi huu kundi la kigaidi la Dola  ya Kiislamu ambalo Boko Haram limetangaza kulitii, lilitangaza kuwa wadhifa wa Shekau ulikuwa umechukuliwa na kiongozi asiye maarufu Abu Mus'ab Albarnawi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment