Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Lady Gaga alitoa ujumbe
muhimu mtandaoni kwa ajili ya kuwaombea dua wahanga wa mzozo wa Syria.Lady
Gaga ambaye ana wafuasi wapatao milioni 64 kwenye mtandao wa jamii wa
Twitter, alisambaza ujumbe huo kupitia video aliyoweka kwenye akaunti
yake kwa hashtag ya #PrayForSyria.
Ujumbe wa Lady Gaga pia
unajumuisha picha ya mtoto wa Syria aitwaye Umran mwenye umri wa miaka 5
aliyeokolewa kutoka kwenye mabaki ya nyumba zilizobomolewa kwa
mashambulizi ya angani mjini Aleppo.
Ujumbe huo pia
uliambatanishwa na picha ya mtoto mwengine mwenye umri wa miaka 6
aitwaye Alex kutoka New York ambaye alimwandikia rais Barack Obama barua
na kutaka kuwa na uhusiano wa karibu na Umran.
Maelezo ya barua
aliyoandika Alex kwa rais Obama na kuchapishwa White House yalisoma
hivi; " Mheshimiwa rais Barack Obama, unamkumbuka mtoto aliyeokolewa
baada ya mashambulizi ya Syria? Tafadhali mleteni nyumbani kwetu.
Tutakusubiria mitaani na bendera na maua ili kukupokea kwa shangwe
utakapowasili. Sisi tutakuwa na uhusiano wa kifamilia. Ndugu yangu mdogo
Catherine hukusanya maua kila siku kwa ajili yake. Shuleni kwetu pia
nina rafiki yangu Omer kutoka Syria. Tutamualika kwenye sherehe ya siku
ya kuzaliwa na tucheze naye michezo ya kitoto. Pia tutamwambia
atufundishe lugha yao na sisi pia tutamfundisha Kiingereza kama
tulivyomfanyia rafiki yetu Aoto kutoka Japan. Tafadhali mwambie ana
rafiki yake mzuri Alex anayempenda kwa dhati. Vile vile mfahamisheni
kwamba Catherine anamtengezea vidude vya kuchezea. Tunasubiria kwa hamu
na ghamu. Shukran. "
Home
BURUDANI
Slider
Lady Gaga atoa ujumbe muhimu mtandaoni kwa ajili ya kuwaombea dua wahanga wa mzozo wa Syria.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment