Image
Image

Afungwa miaka 100 kwa kunajisi watoto kanisani

MWANAMUME aliyenajisi watoto watatu kanisani, amehukumiwa kifungo cha miaka 100 jela baada ya Mahakama ya Kaunti ya Embu nchini Kenya kumkuta na hatia ya kutenda unyama huo. Mtuhumiwa huyo, Harrison Kinyua, alihukumiwa kifungo hicho na Hakimu Maxwell Gicheru baada ya kuridhika na ushahidi kuwa aliwanajisi wanafunzi wawili wa kike wenye umri wa miaka 13 na 10.
Kinyua alitenda unyama huo Desemba 10, mwaka jana katika kanisa hilo lililopo Kijiji cha Kangaru, Kaunti ya Embu.
Wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo, mahakama iliambiwa Kinyua aliwanajisi wanafunzi hao walipokuwa wakirudisha viti walivyokuwa wamechukua kanisani humo.
Alifunga mlango wa kanisa hilo na kisha akawaagiza kulala chini kabla ya kuwanajisi.
Upande wa mashtaka ulisema Kinyua alimfukuza msichana wa tatu aliyekuwa ameandamana na waathirika akidai hakuwa na matiti.
Baadaye aliwapa waathirika Sh 20 (za Kenya) kila mmoja na kuwataka waende kununua chips katika soko la karibu. Lakini wazazi wao waligundua hilo na kuripoti kwa polisi.
Dk. Christine Nyangilo wa Hospitali ya Embu Level Five, aliiambia mahakama kuwa vipimo vilithibitisha wasichana hao wa umri wa miaka 13 na 10 walinajisiwa.
Alisema waathiriwa walipelekwa hospitalini Desemba 10 huku nguo zao zikiwa zimechafuka.
Awali Kinyua alikanusha mashtaka hayo akisema kuwa masaibu yake yalitokana na uhasama uliopo baina yake na familia za waathiriwa.
MTANZANIA:
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment