KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetoa namba maalumu ya
kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mjini Bukoba mkoani
Kagera na kusababisha vifo vya watu 16 na majeruhi kadhaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa
Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza, aliwaomba
Watanzania wote wanaotaka kuchangia waathirikahao kutuma fedha zao
kwenye namba maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya
155990.
“Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na
tunawapa pole waathirika wote na kuungana na wakazi wa Kagera kwa janga
hili na tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia taasisi yetu ya
kusaidia jamii ya Vodacom Tanzania Foundation.
“Tunawaomba Watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia waathirika wa
tetemeko la ardhi watume michango yao na tutahakikisha tunaifikisha
sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako katika mazingira magumu
na wanahitaji msaada wa haraka,” alisema Rwehikiza
Alisema kupitia njia hiyo ya namba maalumu ya ”Vodacom Foundation Red
Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa
fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri
wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo
la mboto jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi
ya uchangiaji ambapo mwisho wa kupokea michango hiyoitakuwa Septemba 24,
mwaka huu ambapo fedha hizo zitawezesha kununua vitu mbalimbali
yakiwemo mahitaji kwa waathirika hao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment