Jumatano
wiki hii, waasi wa kundi la Mai Mai walio nchini DRC walichoma moto
malori 8 kutoka Tanzania na mengine 4 kutoka Kenya na kuwateka madereva
wa malori hayo katika eneo la Namoya mkoani Kivu.
Msemaji
wa wizara ya mambo ya nje nchini DRC Bi. Mindi Kasiga amesema, serikali
za Tanzania na DRC zinajitahidi kuhakikisha kuwa mateka hao wanaachiwa
huru wakiwa salama na kurudishwa Tanzania.
Mwaka
jana mashehe wanane kutoka Tanzania waliotekwa nchini DRC walifanikiwa
kuokolewa kutokana na juhudi za pamoja za serikali za nchi hizo mbili.
0 comments:
Post a Comment